SUZA ni taasisi ya Elimu ya juu ambayo ilianzishwa mwaka 1999 na kuanza kutoa huduma zake rasmi mwaka 2001, kikwa ni miongoni mwa vyuo vikuu vilivyopo nchini, SUZA imefanikiwa katika kuiletea jamii ya kizanzibar na kitanzania kiujumla kwa kujiwekea malengo na mikakati ya kuweza kuibadili jamii ili iweze kutoa mchango wake katika Nyanja za kijamii na kiuchumi kupitia tasnia ya Elimu.
SUZA ni chuo chenye kampasi tatu ambazo ni Beit-el-Rasi ambayo ni majengo ya kilichokuwa chuo cha ualimu Afrika mashariki( Nkrumah) ambacho kinapatikana km 5 tu kutoka Mji Mkongwe, sehemu ambayo imezunguukwa na bahari ya Hindi ambayo ina mandhari nzuri na fukwe ya kuvutia.
Kampasi ya pili ni Vuga iliyokuwa Taasisi ya Kiswahili na lugha za kigeni (TAKILUKI) ambayo ipo katikati ya mji wa Zanzibar, na kampasi ya tatu ni ya Tunguu ambayo ndio kampasi kuu, ni sehemu ambayo ina mazingira tulivu na salama kwa ajili ya kujisomea pamoja na huduma zote muhimu ikiwemo maji, umeme bila ya kusahau vitendea kazi vya kisasa na vyenye ubora
Kwa pamoja tunasema;-
kwa maelezo zaidi kuhusiana na Historia ya SUZA na mengineyo, tembelea www.suza.ac.tz"KARIBUNI ZANZIBAR, KARIBUNI SUZA KATIKA KILELE CHA MAFANIKIO NA KICHOCHEO CHA MABADILIKO YA JAMII"
No comments:
Post a Comment